Tiba ya ugonjwa wa chunusi

Nov

10

2013

Habari yako docta!
Nahitaji ufafanuzi kutokana na tiba ya ugonjwa wa chunusi. (dawa zake za kuziponya) na visababishi vya ugonjwa huo.
Ahsante! Kazi njema.

Tags:

In: Alternative Medicine Asked By: [2 Grey Star Level]
Answer #1

Hello Charldzosias,

Pole kwa kusumbuliwa na chunusi.

Chunusi au acne kwa kitaalam ni ugonjwa wa ngozi unaohusisha tezi za kutengeneza mafuta maalum yanayokuwa kwenye nywele (sebum). Tezi hizi zinapatikana pembeni ya mizizi ya nywele. Kama ndio kwanza unaanza kusoma makala zangu za maradhi ya ngozi itakua vyema nikufahamishe kuwa nywele ni sehemu ya ngozi na kuwa mwili wote wa binadamu una nywele (au vinyweleo) hivyo mwili mzima pia una tezi hizi za mafuta maalum kwa ajili ya nywele.

CHUNUSI HUTOKEA WATU GANI NA KATIKA UMRI GANI?
Mara nyingi chunusi hutokea sana kwa vijana walio kwenye umri ule wa balehe (kati ya miaka 11 na 15). Hii ni kwa sababu wakati wa balehe ndio tezi za kutengeneza mafuta maalum (sebaceous glands) huwa zinaanza kufanya kazi yake.

CHUNUSI HUTOKEAJE?
Kabla ya balehe tezi za kutengeneza mafuta haya maalum kwa ajili ya kulinda nywele na ngozi kwa ujumla huwa zinafanya kazi lakini kwa kiwango cha chini sana na balehe huleta mabadiliko mengi ikiwemo kuongeza maradufu uwezo wa kufanya kazi wa tezi hizi. Tezi hizi huamshwa na kichocheo (homoni ) maalum cha kiume kinachoitwa “testosterone”. Kichocheo hiki (hormone) huanza kuzalishwa wakati wa balehe na ndio kinachoongoza mabadiliko ya kiume (yaani mabadiliko yanayoonekana kwa watoto wa kiume). Kichocheo hiki pia hupatikana kwa watoto wa kike na ni muhimu kwa ajili ya kuweka uwiano wa vichocheo (wanaume pia huwa na vichocheo vya kike).

Ngozi ya mwanadamu ina vishimo vidogo ambavyo huunganisha tezi hizi za mafuta (sebacoues glands) ambazo huwa zipo ndani kidogo ya ngozi na mazingira ya nje ya ngozi. Kupitia vishimo hivi mafuta haya maalum (sebum) hubeba chembe hai zilizokufa kutoka kwenye sehemu za ndani za ngozi na kuzitoa nje ili ziweze kupotea na kuruhusu chembe hai nyingine changa ziweze kukua na kutoa uhai kwa ngozi. Vishimo hivi pia hupitisha nywele ambayo hukua kutokea kwenye mzizi wake.
Chunusi hutokea pale ambapo mirija/vishimo hivi vimeziba kutokana na sababu mbali mbali ambapo mafuta na chembe hai zilizokufa hushindwa kutoka nje kabisa na kuchukuliwa na upepo au kuanguka ardhini. Kuziba huku kwa vishimo hivi maalum husababisha kujazana kwa mafuta, chembe hai zilizokufa kwenye vishimo na kusababisha uvimbe. Uvimbe huu kutokana na kubeba chembe hai zilizokufa huruhusu vimelea vya maradhi kama bakteria kuingia na kusababisha mkusanyiko wa ziada wa usaha na kuongeza ukubwa wa kipele (chunusi).

Vimelea hivi vya bakteria ndio huweza kusababisha chunusi ikawa kubwa na yenye kuuma au isiwe na maumivu yoyote. Bakteria pia husababisha chunusi ikapona na kovu ama bila kovu.

TIBA
Kuna tiba mbali mbali za chunusi la kwa kuanzia tu
Ushauri wangu ni kupunguza kula vitu vyenye Sukari nyingi kama ice cream, chocolate nk Pamoja na vyakula vya mafuta mengi kama Kama vyakula vya kukaanga nk.

Dawa zipo kwa ajili ya kutibu chunusi. Nakushauri kama unaweza basi utembelee kituo cha afya cha karibu na unapoishi ili uweze kuonana na daktari

KINGA DHIDI YA CHUNUSI
Kuna namna mbali mbali za kujikinga ila kwanza ni lazima ufahamu ni nini hasa kimesababisha ukapata chunusi. Hii ni muhimu kwani itakupa mwanga wa namna gani utaweza kupunguza ongezeko la chunusi na kuzitibu zile zililozopo mwilini tayari.
Lengo kubwa wakati unajikinga na upataji au ongezeko la chunusi mwilini mwako ni mojawapo kati ya haya
1. Kufungua vishimo maalum vya kusafirisha mafuta kwenye ngozi
2. Kupunguza idadi ya vimelea vya maradhi vilivyo kwenye ngozi yako
3. Kupunguza wingi wa mafuta unaozalishwa kwenye tezi maalum za kutoa mafuta.

Kinga dhidi ya chunusi inaweza kuchukuliwa katika namna tofauti kama ifuatavyo
Kubadili maisha – Hapa unaweza kuanza kuhakikisha kuwa unapata muda wa kutosha kwa kulala, unakunywa maji mengi na pia kuhakikisha kuwa hugusi chunusi yako kwa kuipasua wala kuikwaruza. Hii inazuia kusambaa kwa vimelea vya maradhi vilivyokwisha vamia kwenye eneo moja la ngozi.

Epuka kabisa kupasua wala kutumbua chunusi kwani ukifanya hivyo unaruhusu vimelea vya maradhi viingie kwenye ngozi na kuweza kusababisha madhara mengine makubwa zaidi. Kama chunusi inasumbua sana na umeamua kabisa kuitoa basi ni bora uchukue sindano nyembamba halafu uiweke kwenye dawa ya kuua vimelea kama vile methylated spirit na baada ya hapo ndio uitumie kupasua/kutoboa chunusi.

• Ili kufungua vishimo vilivyoziba kwenye ngozi inashauriwa kutumia dawa maalum ambazo zinafanya kazi ya kufungua vishimo hivi.

• Ili kuua vimelea vya maradhi kuna dawa ambazo zina uwezo wa kuua vimelea vinavyoleta maradhi kwenye eneo lenye vishimo vilivyoziba yaani kwenye chunusi. Dawa hizi mara nyingi huwa ni za kupaka.

• Ili kupunguza mafuta ya kwenye ngozi mara nyingi inashauriwa kuwa unanawa mara kwa mara kuhakikisha ngozi haibaki na mafuta kwa muda mrefu.

• Huduma za kwenye sehemu za kutengeneza kinamama kama salon huwa wanafanya kitu ambacho kinaitwa facial (fesho). Hii pia inasemekana kuwa husaidia hasa pale ambapo chombo maalum cha kufukiza kinapotumika kwenye ngozi (steaming and deep cleaning).

Matibabu ya chunusi siku zote huhitaji subira kwani matokeo huwa hayaonekani upesi. Matibabu huwa yanahitaji miezi mpaka mitatu kabla matokeo hayajaanza kuonekana. Ni vizuri kusubiri kwanza kabla ya kubadilisha dawa.

Ni matumaini yangu kuwa majibu yangu yamesaidia kuweka angalau mwanga kwenye suala hili la chunusi.

Kwa maelezo Zaidi tunaweza kuwasiliana.
Ninapatikana kwa Namba hizi za Simu

0718311300

Asante sana
Dr Isaac Maro

Answers Answered By: Dr Isaac Maro [66 Blue Star Level]

Answer this Question

You must be Logged In to post an Answer.

Not a member yet? Sign Up Now »

Star Points Scale

Earn points for Asking and Answering Questions!

Grey Sta Levelr [1 - 25 Grey Star Level]
Green Star Level [26 - 50 Green Star Level]
Blue Star Level [51 - 500 Blue Star Level]
Orange Star Level [501 - 5000 Orange Star Level]
Red Star Level [5001 - 25000 Red Star Level]
Black Star Level [25001+ Black Star Level]